Ijumaa 3 Aprili 2026 - 13:00
Ataba tukufu ya Abbasiyya imetangaza kampeni ya kukusanya misaada kwa ajili ya kuwaunga mkono watu wa Iran na Lebanon

Hawza/ Ataba tukufu ya Abbasiyya imeanzisha kampeni ya kukusanya misaada ya wananchi kwa ajili ya kuwaunga mkono watu wa Iran na Lebanon kufuatia matukio ya hivi karibuni katika eneo hilo.

Kwa mujibu wa ripoti ya kitengo cha tarjama cha Shirika la Habari la Hawza, Ataba tukufu ya Abbasiyya imeanzisha kampeni ya kukusanya misaada ya wananchi kwa ajili ya kuwaunga mkono watu wa Iran na Lebanon kufuatia matukio ya hivi karibuni katika eneo hilo.

Katika taarifa iliyotolewa na Ataba tukufu ya Abbasiyya imeelezwa kwamba: Kwa agizo la Hujjatul-Islam wal-Muslimin Sayyid Ahmad Swafi, mwakilishi wa Ayatullah Sistani, inatangazwa kuanza kwa kampeni ya kukusanya misaada kwa ajili ya kuwaunga mkono watu wa Iran na Lebanon, kufuatia matukio ya hivi karibuni ambayo eneo hili linakabiliana nayo.

Katika mwendelezo wa taarifa hiyo imesisitizwa kwamba; juhudi za Ataba tukufu ya Abbasiyya zinafanyika kwa msingi wa maelekezo ya Ayatullah Sistani na kwa lengo la kuimarisha thamani za mshikamano wa kibinadamu na kuimarisha zaidi roho ya umoja miongoni mwa mataifa ya Kiislamu.

Ataba tukufu ya Abbasiyya imewaomba waumini wachukue hatua ya kutoa msaada kupitia njia mbili:

1. Ndani ya Ataba tukufu ya Abbasiyya kupitia ofisi ya idara ya kupokea zawadi, nadhiri na wakfu
(Nambari ya mawasiliano: 07715500066)

2. Kupitia akaunti rasmi zinazohusiana na Ataba tukufu ya Abbasiyya

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha